1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siri za majadiliano ya Mashariki ya Kati nje nje

24 Januari 2011

Hati za siri kuhusu majadiliano ya amani ya Mashariki ya Kati zimefichuliwa na kituo cha habari cha Al Jazeera na kuiweka taswira ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika wakati mgumu mbele ya jamii ya Kiarabu.

https://p.dw.com/p/Quj7
Symbolbild Katar Al Jazeera
Nembo ya Al Jazeera, QatarPicha: DW-Montage

Inasemekana kuwa hati hizo ni kutoka majadiliano yaliyofanywa mwaka 2008, kati ya mawaziri wa nje wa wakati huo, Condoleezza Rice wa Marekani, Tzipi Livni wa Israel, waziri mkuu wa zamani wa Wapalestina Ahmad Qorei na mpatanishi mkuu wa Wapalestina Saeb Erekat.

Al Jazeera imesema kuwa imepata zaidi ya hati 1,600 za siri zinazohusika na majadiliano ya amani ya Mashariki ya Kati yaliyofanywa kati ya Israel na Wapalestina. Kuambatana na hati hizo, mpatanishi mwandalizi wa Kipalestina, wakati huo alipendekeza kuwa Israel ibakie na makaazi yote ya walowezi wa Kiyahudi katika mji wa Jerusalem, isipokuwa eneo moja lililojengwa baada ya Israel kuivamia Jerusalem ya Mashariki mwaka 1967.

Palestinian President Mahmoud Abbas (R) talks with his top aide, Saeb Erekat (L), during a press conference following his meeting with Egyptian President Hosni Mubarak (unseen) in Cairo, Egypt on 28 December 2008. Talks focused on the Israeli attacks against Hamas-ruled Gaza, where over 270 people were killed and more than 900 wounded. EPA/KHALED EL-FIQI +++(c) dpa - Report+++
Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas( kulia) na mpatanishi mkuu Saeb ErekatPicha: picture alliance/dpa

Wiki iliyopita tu, Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas alisema kuwa Jerusalem ni yao na hilo wala si suala la kujadiliwa. Mpatanishi mkuu wa Wapalestina, Saeb Erekat alipohijiwa na Al Jazeera alisema, serikali ya Wapalestina haina cho chote cha kuficha na ameipuza ripoti hiyo kama ni uwongo mtupu. Kwa sasa, majadiliano ya amani yamekwama. Wapalestina wanakataa kurejea kwenye meza ya mazungumzo mpaka Israel itakapositisha ujenzi wa makaazi ya Wayahudi katika maeneo ya Waarabu.