1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Waandamanaji wapambana na polisi nchini Iran

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4o

Mamia ya watu wamepambana na polisi nchini Iran katika maandamano yanayomuunga mkono kiongozi wa kidini anaependekeza kutenga dini na serikali. Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kulitawanya kundi la kama watu 200 mbele ya nyumba ya Ayatollah Mohammad Kazemeini Boroujerdi katika mji mkuu Tehran.Boroujerdi,alie kiongozi wa kidini wa ngazi ya juu,anaongoza kundi linalotoa wito wa kutenganisha dini na siasa-mada iliyo mwiko nchini Iran.Waandamanaji hao wamedai kuwa baadhi ya wafuasi wa Boroujerdi wametiwa ndani na wanataka waachiliwe huru.