1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel itawacha ujenzi kwenye Ukingo wa Magharibi?

15 Septemba 2010

Viongozi wa Israel na Palestina wameshindwa kufikia makubaliano yoyote katika suala la ujenzi wa makazi ya Wayahudi kwenye Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/PCGt
Benjamin Netanyahu,Hillary Clinton na Mahmoud AbbasPicha: AP

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas walikutana Sharm-el Sheikh nchini Misri katika awamu ya pili ya mazungumzo ya ana kwa ana yaliyo na azma ya kuisaka amani ya kudumu ya Mashariki ya Kati.Hata hivyo,mjumbe maalum wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati George Mitchell anasisitiza kuwa msimamo wao kuhusu suala hilo haujabadilika.

Barack Obama mit Benjamin Netanyahu und Mahmoud Abbas NO FLASH
Viongozi wa Israel na Palestina walipokutana Washington kwa mara ya kwanza ana kwa ana baada ya zaidi ya mwaka mmoja.Picha: AP

Mjumbe huyo aliendelea kueleza kuwa mazungumzo hayo sharti yapewe uzito na yawe ya faragha.Itakumbukwa kuwa muda uliowekwa wa kuusitisha ujenzi wa makazi ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi utamalizika mwishoni mwa mwezi huu.Kwa upande wake Rais Mahmoud Abbas ametoa vitisho kuwa huenda akajiondoa kwenye meza ya mazunguzumzo endapo ujenzi huo utaanza tena upya.Hii leo,Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton anatazamiwa kukutana na wawakilishi wa Israel na Palestina kwenye kikao cha pamoja kitakachofanyika mjini Jerusalem.