Mazungumzo ya amani yatafana,yasema Ujerumani
22 Agosti 2010Bibi Merkel aliupongeza uamuzi huo wa kuyaanzisha upya mazungumzo hayo ya amani yaliyokwama mwaka 2008,pindi baada ya israel kuuvamia Ukanda wa Gaza.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuanza rasmi ifikapo tarehe mbili mwezi wa Septemba ijapokuwa wanasiasa wa pande zote mbili husika wameshatoa tahadhari kuwa huenda kukatoea vikwazo.Kulingana na msuluhishi mkuu wa Palestina Saeb Erakat,upande wao utajiondoa kwenye vikao ikiwa Israel itaendelea na ujenzi wa makazi yake katika eneo wanalolikalia.Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa mazungumzo hayo ni nafasi ambayo haipaswi kupotezwa.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton alitangaza siku ya Ijumaa tarehe hiyo ya waIsrael na wapalestina kuanza mazungumzo ya moja kwa moja kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 20. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa gazeti la Marekani la New York Times.
Muda wa mwaka mmoja
Gazeti hilo limewanukuu maafisa wawili ambao majina yao hayakutajwa, walioarifiwa juu ya hali hiyo, wakisema Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Palestina Mahmud Abbas, wamekubaliana kuweka muda wa mazungumzo uwe mwaka mmoja.
Rais Barack Obama wa Marekani anatarajiwa kuwaalika Netanyahu na Abbas mjini Washington mapema mwezi ujao wa Septemba kuanza mazungumzo, yatakayo zingatia sehemu ya mwisho ya masuala tete ikiwa ni pamoja hatima ya mji wa Jerusalem pamoja na kurejea kwa wakimbizi wakipalestina.
Kurejea katika mazungumzo, itakua ni hatua ya kwanza muhimu ya mafanikio kwa utawala wa Obama katika juhudi zake za kuyafufua mazungumzo ya amani ya Mashariki ya kati.
Mazungumzo ya ana kwa ana baina ya Israel na Wapalestina yamekwama kwa karibu miaka miwili, licha ya shinikizo la Marekani kwa pande zote mbili.
Duru ya mwisho ya mazungumzo ya moja kwa moja ilivunjika , pale Israel ilipofanya hujuma ya wiki tatu ya kijeshi katika ukanda wa Gaza Desemba 2008 katika jaribio la kuzuwia mashambulio ya maroketi ayaliofanywa na wanaharakati wa chama cha Hamas kinachotawala eneo hilo.
Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani imeonyesha kuwepo kwa matumaini juu ya mazungumzo ya ana kwa ana yanayopangwa kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao.
Msemaji wa wizara hiyo Philip Crowley aliwaambia waandishi habari kwamba Waziri Clinton ameshauriana na Waziri wa mashauri ya kigeni wa Jordan Nasser Judah na Waziri mkuu awa azamani wa Uingereza Tony Blair ambaye ni mjumbe wa kundi la pande nne zinazohusika na suala la mashariki aya kati ambazo ni Marekani, Urusi, Umoja wa mataifa na Umoja wa Ulaya.
Ujenzi wa makazi una utata
Maafisa wa Palestiana wamesema hatua yoyote mpya lizima iwe katika zingatio la taarifa iliotolewa na kundi hilo la pande nne mjini Moscow na ambayo imeitaka Israel kusitisha ujenzi wa makaazi na hakikisho kwamba amazungumzo hayo yatafikia mkataba wa mwisho katika kipindi cha miaka miwili. Lakini vyombo vya ahabari nchini Israel viliripoti wiki hii kwamba wajumbe saba katika baraza la mawaziri la Israel, waliikataa taarifa ya kundi hilo.
Israel ikashikilia iko tayari kuingia kwenye mazungumzo, lakini bila amasharti yoyote,
Netanyahu na Abbas waliizuru Washington mnamo miezi ya karibuni kwa mazungumzo tofauti na rais Obama, huku ikulu ya Marekani ikitoa wito kwa pande hizo mbili kuharakisha hatua ya kuanza mazungumzo ya moja kwa moja.