1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Premier League:Arsenal yabanwa mbavu, Chelsea yamtuliza shetani kichwani

30 Desemba 2010

Chelsea jana ilimtuliza shetani wake kichwani baada ya kuifunga Bolton bao 1-0,lakini Arsela walilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Wigan Athletic.

https://p.dw.com/p/zrUL
Didier DrogbaPicha: picture-alliance/dpa

Sare hiyo ambayo Arsenal imeipata imeifanya ifikishe pointi 36, ikiwa ni pointi mbili nyuma ya vinara Manchester United na Manchester City. Chelsea wao pamoja na ushindi huo imeendelea kubakia katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 34.

Kabla ya mechi yake na Bolton Chelsea walikuwa katika chagizo kubwa la kuwapa matumaini washabiki wao ambao wameishuhudia timu hiyo ikipepesuka katika mechi kadhaa za hivi karibuni, ikiwemo ya mwanzoni mwa wiki ilipochapwa mabao 3-1 na Arsenal.

Nayo Arsenal ilishindwa kubaini wapi zilipo mbinu walizotumia kuwaadhibu Chelsea, pale walipolazimishwa sare ya mabao 2-2 na Wigan ambayo walicheza pungufu katika dakika 14 za mwisho baada ya mchezaji wao kutolewa kwa kadi nyekundu.

Nayo Liverpoool ilichapwa bao 1-0 na Wolverhampton Wanderers. Wolverhampton ambayo ndiyo inayokamata nanga ya ligi hiyo kuu ya Uingereza ikiwa na pointi 15, ilistahili kushinda mechi hiyo kutokana na kucheza kwa nguvu na ari kubwa.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters

Mhariri:Josephat Charo