1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waongeza shinikizo dhidi ya Gbagbo

Abdu Said Mtullya30 Desemba 2010

Watu 61 wa Gbagbo wapigwa marufuku kuingia Ulaya.

https://p.dw.com/p/zrKu
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamepania kumtaka Gbagbo ang'atukePicha: AP

Umoja wa Ulaya umeimarisha shinikizo la kumtaka rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast aondoke madarakani.

Kwa mujibu wa taarifa ya tume ya Umoja huo, idadi ya watu wa Gbagbo waliopigwa marufuku kuingia katika nchi za Umoja huo itaongezeka kutoka 19 na hadi 61.

Wakati huo huo wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imearifu kuwa Umoja wa Ulaya utawatambua wajumbe wa kiongozi wa upinzani Alassane Outtara kuwa wawakilishi wa Ivory Coast.Jumuiya ya kimataifa inamtambua bwana Outtara kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika nchini Ivory Coast mwezi novemba.

Wakati huo huo jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi Ecowas imearifu kuwa wiki ijayo itachukua hatua zaidi ili kujaribu kuleta suluhisho la mgogoro wa kisiasa unaoikabili Ivory Coast.

Hapo jumanne ujumbe wa marais watatu kutoka jumuiya ya Ecowas ulishindwa kumshawishi Gbagbo aondoke madarakani.