1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Ecowas waondoka Ivory Coast.

Abdu Said Mtullya29 Desemba 2010

Mazungumzo ya kuutatua mgogoro wa kisiasa Ivory Coast yataendelea karibuni.

https://p.dw.com/p/zqwT
Anaetambuliwa kuwa mshindi wa uchaguzi Alassane Outtara na mkewe.Picha: Picture alliance/dpa

Mazungumzo kati ya kiongozi wa Ivory Coast Laurent Gbagbo na ujumbe wa marais watatu kutoka jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, Ecowas yamemalizika mjini Abidjan. Rais wa Cape Verde aliekuwamo katika ujumbe huo Pedro Pires amesema mwenyekiti wa jumuiya ya Ecowas ataandaa tarehe ya kukutana tena na Gbagbo.Lakini ameeleza kuwa mkutano huo utafanyika hivi karibuni. Ujumbe wa jumuiya ya Ecowas wa marais kutoka Sierra Leone,Benin na visiwa vya Cape Verde ulikuwa Abidjan kwa madhumuni ya kumshawishi Gbabo aondoke madarakani kwa hiari.

Marais hao sasa wataenda Abuja kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa jumuiya ya Ecowas ,rais Goodluck Jonathan wa Nigeria.

Wakati huo huo rais Gbagbo ametishia kuvunja uhusiano wa kibalozi na nchi zilizowatambua mabalozi walioteuliwa na kiongozi wa upinzani Alassane Outtara anaetambuliwa na jumuiya ya kimataifa kuwa mshindi wa uchaguzi.

Habari zaidi kutoka Abidjan zinasema kuwa msafara wa wanajeshi 22 wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani nchini Ivory Coast ulishambuliwa. Askari mmoja alijeruhiwa na gari moja la askari hao lilipigwa moto.