1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arsenal yaisambaratisha Chelsea

28 Desemba 2010

Chelsea jana ilichapwa mabao 3-1 na Arsenal na hivyo kuzidi kupoteza matumaini ya kutetea ubingwa wao wa ligi kuu ya Uingereza.

https://p.dw.com/p/zqc4
Kocha wa Arsena Arsene WengerPicha: picture-alliance/ dpa

Yalikuwa ni mabao ya Alex Song, Cesc Fabregas na Theo Walcott yaliyopeleka majonzi Stamford Bridge.

Arsenal sasa imefikisha pointi 35, nyuma ya vinara Manchester United wenye pointi 37, huku Chelsea ikibakia katika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 31.

Kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti alikiri kuwa hali si nzuri kwao, na kwamba ni lazima waamke, ingawaje hana wasiwasi.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters

Mhariri:Josephat Charo